Mwa...naume sister mambo
Sister mambo kwa yesu
Mwanume Sister samahani . . . unampenzi
Sister hapana sihitaji mpenzi!
Mwanaume mwanzo 218 mungu akasema sio vema mwanaume akabaki peke yake nitamfanyia msaidizi.
Sister Lakini Mimi sikupendi . . . .. . nampenda yesu!
Mwanaume 1yohana 420 MTU akisema anampenda mungu naye humchukia ndugu yake ni mwongo kwamaana asiyempenda ndugu yake amwonaye atampendaje mungu asiyemwona
Sister Nitaaminije kwamba maneno yako uongeayo ni kweli
Mwanaume mathayo 1234-36mtu mwema katka akiba njema ya moyo wake hutoa mema na MTU mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya
Ila mimi Kinywa changu huongea maneno yaliyoujaza moyo wangu
Sister nitaaminije hayo uongeayo ni kweli
Mwanaume Marko 1341 mbingu na nchi zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe
Sister mbona wako wako wanawake wengi sana kwanini umeniambia Mimi tu
Mwanaume mithali 3129 binti za watu wengi wamefanya mema lakini wewe umewapita wote!
Sister ni nini kilichokufanya unipende mimi na si wengne nimekuvutia nini
Mwanaume wimbo bora 47 uu mzuri sana ndani yako Hamna hila
Sister ni kweli Mimi sio mzur wa kupendwa na wewe !!
Mwanaumemithali 3130 upendeleo hudanganya na uzur ni ubatili Bali mwanamke amchae bwana ndiye atakaye sifiwa
Sister ni nini kitatokea nikikubali na kusema ndio!
Mwanaume mwanzo 24 mwanaume atawaacha wazazi baba na mama ataambatana na mkewe na hao wawili hawatakuwa wawili tens Bali mwili mmoja.
Sister imekuwaje unajua sana maandiko utafikir mchungaji
Mwanaume Joshua 18 kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwenu Bali yatafakali maneno yangu mchana na usiku ndipo utakapo zifanikisha njia zako
Sister yaah!! Nakuona unampenda sana mungu
Mwanaume zabur 348 onjeni mwone kuwa bwana ni mwema heri MTU yule anayemtumainia
Sister. mmmh bas nipe muda nifikirie kuhusiana na hili
Mwanaume wafilip 48 hatimaye mambo yeyote yaliyo kweli ya staa ya haki yenye kupendeza yenye sifa njema na wema wowote yatafakalini hayo
Sister nimekubali nakupenda nami pia
Mwanaume ufunuo 2221 Amen
TOA MAONI YAKO NA SHARE UMEIONAJE

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni